BARNABAS WA THT MBIONI KUPAKUA ALBAM MPYA

BARNABAS

CHIPUKIZI aliyejuu kwa sasa katika medani ya bongo fleva Barnabas toka Tanzania House of Talent (THT) yupo mbioni kukamilisha albamu yake binafsi itakayokuwa na nyimbo sita.

Mkali huyo anayetikisa tangu alipoibuka kwenye game amesema kwamba katika albamu yake hiyo anapenda amshirikshe mkali nguli wa bongo fleva Judith Wambura maarufu kama ‘Lady Jay dee’.
Baranabas amevitaja vibao vitakavyokuwemo kwenye albamu hiyo ni pamoja na pamoja na ‘Tulizana’, ‘Mwenyekiti wa Kamati’, ‘Kweli Nimegundua’, ‘Mke wa Mtu’, ‘Kichwa Changu’ na ‘Nitajaribu’.
Awali Barnabas alitoa albamu ya pamoja na swahiba wake Amini Mwinyimkuu ikijulakana kama ikiwa na vibao kama ‘Wrong Number’, ‘Njia Panda’, ‘Simu ya Kamera’, ‘Robo Saa’, ‘Soo Soo’, ‘Mama Vanessa’, ‘Mbalamwezi’, ‘Nivumilie’ na nyinginezo

Comments