BANKA, KASEJA, MGOSI NDANIO YA KOMEDI

KUTOKA KUSHOTO JUMA KASEJA, MUSA MGOSI NA MOHAMED BANKA

HAIJAWAHI kutokea, kwa mara ya kwanza katika historia ya sanaa nchini wasukuma kandanda mahiri wa timu ya soka ya Simba Mussa Hassan Mgosi, Juma kaseja na Mohamed Banka wameonyesha vipaji vyao vya ziada baada ya kushiriki katika vichekesho.
Wachezaji hao wameigiza katika vichekesho vya ‘Futuhi’ vinavyorushwa katika kituo cha Televisheni cha Star kilichopo jijini Mwanza ambapo wamerekodi moja ya mchezo utakaokuwa hewani hivi karibuni.
Mmoja ya watu wa karibu wa wachezaji aliiambia Sayari kwamba nguli hao wa kandanda walipata wasaa huo wa kuonesha vipaji vyao vya ziada wakati timu ilipokuwa imepiga kambi jijini Mwanza ikijiandaa na Ligi kuu ya Vodacom.
“Yaani huwezi kuamini kama ndio hao unaowafahamu, jamaa wana vipaji ile mbaya, yaani mashabiki wa kipindi hicho wasiache kuangalia na watawakubali kwa kweli”, Alisema.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Mgosi na Banka kujitosa katika sanaa, lakini kwa Kaseja ‘kipa bora wa ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita’ ni mara yake ya tatu kwani mapema mwaka jana alishiriki kama muigizaji wa kawaida katika filamu za Soka la Bongo na Septemba 11.

Comments