AFC YA ARUSHA YAONA MWEZI KATIKA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA

AFC ya Arusha jana iliona mwezi baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 3-2 katuika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tabnzania Bara iliyopigwa katika uwanja wa Sheik Amri Abeid mjini Arusha.
Mtibwa nayo ilitoka sare ya bao 1-1 na Toto Afrika ya Mwanza, mechi ilichezwa Manungu, Morogoro.
Kagera Sugar iliifunga Polisi Tanzania bao 1-0, mechi ilipigwa dimba la Kaitaba, Kagera.
Nao Ruvu Shooting na AQfrican Lyon waliokuwa wakikipiga katika dimba la Jamhuri, Morogoro walitoka suluhu ya bila kufungana.

Comments