ZAWADI KIBAO ONYESHO LA FM ACADEMIA MBAGALA IJUMAA

RAIS WA BENDI YA FMA ACADEMIA NYOSHI EL SAADAT KUSHOTO

WAANDAJI wa Onesho la Bendi ya FM Academia wazee wa Ngwasuma zawadi kwa
washindi watakaibuka katika shindano maalum la kucheza mitindi ya bendi hiyo,
kwenye utambulisho wa bendi hiuyo utaofanyika kesho kwenye Ukumbi wa
Nawina Resort Mbagala Kuu Dar es Salaam.
Mratibu wa Onesho hilo Zahor Said, alisema kuwa usiku huo maalum wa Ngwasuma utakuwa na burudani mbalimbali ambazo zitausindikiza utambulisho huo.
Said alisema watafanya utambulisho huo kwa kusindikizwa na vikundi vya unenguaji vya kiduku.
Alisema utambulisho huo wa albamu ya Vuta nikuvute utakuwa chini ya Rais waNyoshi El Saadat watapiga nyimbo zote 11 zilizopo kwenye Albamu hiyo ikiwa ni pamoja na nyimbo za zamani.
Nyimbo zilizobeba albamu hiyo kuwa ni Heshima kwa Wanawake ambayo ilipata tunzo mwaka jana,Mwili wangu, Usiku wa juma tano na Jasmini.
Nyimbo zingine ni Angalia shida yangu,Mgeni,Heiken Ngwasuma,Moses Katumbi,Fadhila kwa mama Intro Ngwasuma Mathematics na vuta ni kuvute ambayo imebeba jina la albam.
Usiku huo umedhaminiwa na Henkein Bear, Kampuni ya Inoch, Blog za JaneJohn5, Mamapipiro na Full Shangwe.

Comments

  1. Huyu Nyoshi anatisha sana!!! je, hana ndugu au marafiki watakaomshauru awache kujichubua ngozi. Au wanaogopa kumwambia ukweli? Kujichubua ngozi ni dhambi. Naomba Watanzania wenzangu wa kila kabila, rangi na dini tusijichubue ngozi zetu. Tuachane na kasumba ya kujidharau. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CCM!!!!! Amen. Mr. A.

    ReplyDelete

Post a Comment