YANGA BADO YAKOMALIA UWANJA WA TAIFA

MWENYEKITI WA YANGA LLOYD NCHUNGA KUSHOTO , PAMOJA NA OFISA HABARI WA TIMU HIYO LOUIS SENDEU WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIONI HII.

UONGOZI wa klabu ya Yanga umepokea kwa masikitkio makubwa taarifa za Serikali kutotumia uwanja wa Taifa kwa michezo yake ya ligi Kuu Tanzania bara.

Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema awali Yanga ilishatoa msimamo wake kwa TFF kuwa ingependa kuutumia uwanja wa Taifa kufuatia uwanja wa Uhuru kufungwa kwa ajili ya matengenezo.
Katika kikao kilichofanyika makao makuu ya TFF ambacho kilishirikisha klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu miongoni mwa klabu vilivyotoa pendekezo la kutumia viwanja mbadala na uwanja wa Uhuru ni klabu za Simba ambayo ilitangaza kutumia uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na Azam FC ambayo nayo ilitangaza kuutumia uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Kufuatia mchakato huo klabu ya Yanga iliitaarifu TFF kuiombea uwanja wa Taifa kwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutumika katika michuano ya Ligi Kuu.
Makubaliano katika mkutano huo klabu ya Yanga ndio pekee iliyojitokeza katika mazungumzo na Wizara ambapo miongoni mwa makubaliano hayo ni pamoja na kupunguzwa kwa asilimia 10 badala ya 20, sh 3000,000 za kuwalipa Wachina, sh 1,900,000 gharama za usafi wa uwanja na sh 450,000 gharama za matayarisho ya uwanja kabla ya mechi.
Iwapo juhudi za Yanga kuutumia uwanja wa Taifa zitagonga mwamba, wanatarajia kuuchagua uwanja wa Jamhuri wa mjini Morogoro kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu.

Comments