WASHIRIKI VODACOM MISS TANZANIA WAGAWA VYANDARUA HOSPITALI KISARAWE

 Mrembo anaeshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania Gloria Mwanga akimkabidhi Ashura Amri chandarua kwa niaba ya mwanae Juma Mohamed aliyelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe.Msaada huo unaunga mkono harakati za kutokomeza malaria kupitia kampeni yake ya zinduka.


Mrembo anaeshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania Fatma Ibrahim akimkabidhi Asha Rashid chandarua kwa niaba ya mwanae Rashi Abdalah aliyelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe.Msaada huo unaunga mkono harakati za kutokomeza malaria kupitia kampeni yake ya zinduka.

01. Balozi wa kampeni ya malaria haikubaliki mwanamziki Diamond pamoja na warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania wakimkabidhi chandarua Rukia Shaibu aliyelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe.Msaada huo unaunga mkono harakati za kutokomeza malaria kupitia kampeni yake ya zinduka.

KATIKA kuunga mkono kauli mbiu ya Rais Jakaya Kikwete ya kupinga ugonjwa wa Malaria inayosema ‘Malaria Haikubaliki’ warembo wa Vodacom Miss Tanzania wamegawa vyandarua 200 kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ili kusaidia kuangamiza ugonjwa huo.

Wakikabidhi vyandarua hivyo hospitalini hapo warembo hao walisema wanafahamu juhudi za serikali katika kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo na ndio maana wanajitoa ili kuihamasiaha jamii kutumia vyandarua katika kipindi chote cha mwaka jambo litakalosaidia kupunguza vifo kutokana na ugonhjwa huo.
“Tumegawa vyandarua hivi kwa watoto wachanga, akina mama wenye magonjwa mbalimbali na kwenye wodi ya watoto ili kuhamasisha matumizi ya vyandarua katika kipindi chote cha mwaka na tumewatumia akina mama na watoto kwani wao ndio wanaoathirika zaidi pale kutokana na majukumu yao ya kifamilia,” alisema mrembo Jhalli Murey.
Akipokea msaada huo Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Dk Elly Helela alisema kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali wamekuwa wakiendelean katika vita hiyo ya kupambana na Malaria na kwamba wanawashukuru wadau wote wanaojitokeza katika kuwaungfa mkono.
Akifafanua zaidi Dk Helela alibainisha kwamba wilayani kwake angalau wameweza kupunguza kiasi cha maambukizi kutoka aslimia 69 hadi kufikia 53 jambo alilosema limechangiwa na misaada na uhamasishaji kama walivyofanya Vodacom Tanzania.
“ Hii ni vita ambayo jamii nzima haina budi kushiriki katika kuishinda, Vodacom Tanzania kupitia warembo wenu leo mmeonesha njia. Ni matumaini yangu kwamba kampuni zingine zitaiga mfano wenu kwa kutusaidia vyandarua vilivyotiwa dawa kwani mamalia haikubaliki,” alisema Dk Helela.
Kwa upande wake Nector Foya ambaye ni Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania alisema lengo la kuwatumia warembo hao kugawa vyandarua ni katika kuikumbusha jamii kwamba malaria haikubaliki na inaweza kuepukika kama yalivyo magonjwa mengine.
“Kutokana na hilo kampuni yetu haitoi vyandarua tu ili angalau kupunguza kiwango cha malaria kama alivyosema Dk Helela, dhamira yetu ni kuona ugonjwa huu unatokomea kabisa nchini kwani kama alivyosema rais Kikwete malaria haikubaliki hivyo jamii izinduke kuutokomeza,” alisema Foya.
Naye msanii Mwasiti Almasi ambaye ni balozi wa mradi wa Zinduka alitoa rai kwa jamii kuikataa malaria kwa kusema hapana na kwamba kizazi cha sasa kiwe cha mwisho kuugua malaria jambo alilosema litasaidia kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.
Wakiwa mkoani Kilimanjaro warembo hao 30 walitoa zaidi ya vyandarua 100 katika Hospitali ya Marangu kama sehemu ya ushiriki katika kuihudumia na kujifunza shughuli za kijamii.

Comments