WACHEZA KIKAPU WA TIMU YA AFRIKA WATUA FREE MEDIA

KUTOKA KUSHOTO ALPHAEUS KISUSI , TAHER ABDULRAHMAN CHILIVINGOSOS  AMBAYE YUPO KWENYE KAPU, SUNDAY EDWARD NA EVANCE DAVIES.




DEODATUS MKUCHU AKA MZEE WA KWA ALIMBOA, MHARIRI WA MICHEZO WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA

SUNDAY EDWARD HUYU NI MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KATIKA SEKONDARI YA OYESTERBAY.

TAHER ABDULRAHMAN CHILIVINGOS HUYO AMEMALIZA KIDATO CHA NNE ST.MARY'S HIGH SCHOOL.

EVANCE DAVIES HUYU ANASOMA KIDATO CHA NNE, FILBERT BAYI SEKONDARI.

ALPHAEUS KIKUSI, HUYU AMEMALIZA KIDATO CHA SITA, ACADEMIC INTERNATIONAL SCHOOL
WACHEZAJI chipukizi wa mpira wa kikapu toka hapa nchini ambao wameteuliwa  kuunda kikosi cha  timu ya  Afrika jana walitembelea ofisi za free media zinazochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari na kufanya mazungumzo ya kina na Mhariri wa Michezo wa Tanzania Daima, Deodarus Mkuchu.
Kikosi hicho Novemba mwaka huu kitakwenda nchini Marekani kushiriki mashindano na mafunzo maalumu kwa lengo la kuinua kiwango cha mchezo huo Tanzania na Afrika.

Vijana hawa ni matunda ya programu ya siku mbili iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa kampuni ya Coca Cola Kwanza Bottlers na kushindanisha vijana 32 wa umri wa chini ya miaka 17.
Kliniki hiyo ilifanyika chini ya wakufunzi Steve Smith na Martin Conlon kutoka Marekani wakisaidiwa na makocha wazawa, Bahati Mgunda, Manaseh Zablon, Dasse Makula na Pasco Nkuba.

Comments