WABUNIFU WA MAVAZI CHIPUKIZI 16 WATINGA NUSU FAINALI YA 'SWAHILI FASHION WEEK'

MAJAJI KAZINI KUTOKA KUSHOTO MAMA NSAO SALUA, CHARLES WASHOMA KATI NA MANJU MSITA

HII NI BAADHI YA MICHORO YA WASHIRIKI WA KINYANG'ANYIRO

Majina ya wabunifu 16 wenye vipaji ambao wataingia katika nusu fainali na kushindania zawadi ya mwaka katika onyesho kubwa la wiki la mavazi Swahili Fashion Week 2010 wapatikana.
Uchaguzi wa wabunifu wa mavazi wanaochipukia umefanyika Septemba 29 katika hotel ya Southern Sun jijini Dar es salaam, ambapo majina 16 yalichaguliwa na jopo la majaji watatu ambao ni Manju Msitta kutoka Smart Afrika Design Label, Charles Washoma, CEO of African Life assurance and One of Dar es Salaams fashionable man na Director of arts Nsao Shalua of Baraza la Sanaa la Taifa (National arts Council).
Wabunifu hao 16 waliochaguliwa katika nusu fainali, kwa mara nyingine tena watachuana katika mchujo wa kuwapata wabunifu wa mavazi wanaochipukia wanane (8) ambao watashindana katika kuonyesha kazi zao katika onyesho kubwa la wiki la mavazi Swahili Fashion Week litakayofanyika mwezi wa Novemba mwaka huu.
Mratibu wa Swahili Fashion Week, Ndugu Washington Benbella amesema kuwa “Muitikio umekuwa ni mzuri, ari na hamu imeonyesha vipaji vya hali ya juu vya ubunifu wa mavazi ambavyo vipo hapa nchini, lakini kwa wale ambao hawakupahatika kupata nafasi ya kuchaguliwa wasiishie hapa na wasikate tamaa bali waendelee na kuhakikisha kwamba wanafanikiwa na kufikia malengo yao”
Wabunifu wa mavazi wanaochipukia waliofanikiwa kuingia nusu fainali ni pamoja na Zarina Suleiman, Pooja Narendrakumar Jeshang, Abduel Urasa, ShaibMfaume, Annette Ngogi, Mwajabu Sadiki, Diana Malenge, Mgece Makory, Omary Bundalah, Kelvin Boniface, Subira Rahma Wahure, Nadia. A. Ahmed, Angelina Muna, Jacqueline Chipeta, Bami Musese na Grace Kijo.
Majaji walikuwa na kazi ya ziada, kwani walikuwa makini katika kuangalia mambo mbalimbali ili kuweza kupitisha majina ya wabunifu wa mavazi wanaochipukia, kwani walilazimika kualiangalia uwezo katika ubunifu na kuchora, kwa kiasi gani mchoro unavitia, rangi iliyotumika katika mchoro na mambo mbalimbali yanayohusiana na ubunifu kwa ujumla.
Sahili Fashion Week ni jukwaa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.
Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kwamba sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa kwa nchi za Afrika Mahariki.
Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week imekuwa ikifanyika, ambapo kwa mwaka huu itafanyika November 2010, Dar Es Salaam , Tanzania .
Shindano hili linafanyika kwa mwaka wa tatu sasa, halina kikwazo cha umri, na linatoa fursa kwa watu wote wanaoamini kwamba wana kipaji cha ubunifu, na wanataka kuwa wabunifu. “Swahili Fashion Week ni jukwaa bora kwa wabunifu kuonyesha uwezo wao wa ubunifu na kuibua sindano la wabunifu wapya, ni jukwaa linalowawezesha watu kufikia malengo yao ”, aliongeza Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week.

Saphia Ngalapi
Media & PR Manager
Mustafa Hassanali
PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania
105 Kilimani Road, Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania
(opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy)
Tel : +255 (0)22 266 8555
Mobile : +255 (0)712 099 834
Mail : media@mustafahassanali.net
Web : www.mustafahassanali.net
http://www.swahilifashionweek.com/
http://www.harusitradefair.com/
http://www.twende.info/

Comments