WAAMUZI WANNE WA LIGI KUU YA VODACOM JELA MIEZI SITA

FLORIAN KAIJAGE,OFISA HABARI WA TFF
KAMATI ya Mashindano ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) iliyokutana juzi imewasimamisha miezi sita waamuzi Ronald Swai na msaidizi wake namba mbili Samuel Mpenzu baada ya kushindwa kutafsiri sheria za mchezo kati ya Yanga na Kagera Sugar uliochezwa Septemba 15 katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro na kusababisha Yanga kufunga bao la kwanza.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage waamuzi hao wamefungiwa kufuatia kanuni ya 26 (1a) ambako Kamishina wa mchezo huo Babu Ng’ombo wa Lindi amefungiwa miezi 12 baada yakushindwa kuandika taarifa sahihi za mchezo huo ambako matukio yaliyotokea baada ya mchezo huo baada ya kumalizika kwa mchezo huo yatawasilishwa katika kamati ya nidhamu.
Kaijage alisema TFF imeziandikia barua za Onyo klabu za Ligi Kuu Tanzania bara baada ya mchezo kati ya Yanga na AFC uliuochezwa Septemba 10 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kikundi cha ushangiliaji cha Yanga kilisababisha kero katika jukwaa Kuu.
Katika mchezo kati ya Simba na Azam uliochezwa Septemba 11 katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, mwamuzi Mathew Akrama na msaidizi wake Frank Komba nao wamefungiwa miezi sita baada ya kushindwa kutafisiri sheria kwa kupata alama za chini kutoka kwa kamishina Charles Mchau.
Mchezo kati ya Majimaji ya Songea na African Lyon uliochezwa Agosti 28 katika uwanja wa Majimaji, Majimaji ilichelewa kuingia uwanjani kwa dakika 15 na kuchelewesha mchezo kuanza, hivyo Majimaji imetozwa faini ya shilingi 300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 13 (12).

Comments

  1. Ndipo hapo watu wanapojikanyaga, sheria inasema kula na kijiko wewe unakula na kisu!

    ReplyDelete

Post a Comment