USIKU WA KANGA ZA KALE WAIVA


ASIA IDAROUS, MKURUGENZI WA FABAK FASHION
MKUU wa Wilaya ya Temeke, Chiku Galawa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ‘Usiku wa Kanga za Kale’ utakaofanyika Oktoba mosi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashion, Asia Idarous, tamasha hilo litashirikisha wabunifu wa mavazi na wadau mbalimbali, wakiwemo kina mama na kina baba watakaopanda jukwaani kuonyesha mavazi ya kanga na vionjo.
Idarous alisema tamasha hilo litasindikizwa na burudani kutoka kundi la Jahazi Modern Taarab, waimbaji nyota Khadija Kopa, Rukia Ramadhani, Sabah Salum Muchacho na Baby Madaha.
Aidha, Idarous alitaja viingilio katika usiku huo kuwa ni shilingi 20,000 kwa viti maalumu ‘VIP’ na shilingi 10,000 kwa viti vya kawaida, ambako tiketi zinapatikana Fabak Fashions, Zizou Fashions na Baco Deco Opp.
Usiku huo umedhaminiwa na Antelope Tours Ltd, Michuzi Blogsports, Vayle Spring, Big Solution, Evernight, Myriad, Channel Ten, Magic FM, Clouds FM, Shear Illusion, Mlimani TV, Iview Photography, TBC, Full Shangwe blogspot, Jiachie, 8020 blogspot na Gema Sound.

Comments