USAIN BOLT ATAKA KUKIPIGA MANCHESTER UNITED


MWANARIADHA mwenye kasi zaidi duniani, anayeshikilia rekodi ya dunia ya mita 100 na 200, Usain Bolt wa Jamaica, amesema anataka kujikita kwenye soka na ataka asajiliwe Manchester United ya England.
Bolt, aliyeweka rekodi katika mbio za Olimpiki za mwaka 2008 zilizofanyika Beijing, China, alisema kuwa soka analifahamu na aliwahi kukipiga alipokuwa shule ya sekondari, akicheza kiungo namba sita na wingi ya kushoto.
Alisema kuwa pamoja na kukimbia lakini amekuwa akishabikia soka na klabu anazozipenda ni United na Real Madrid ya Hispania.“Sitanii lakini ni kweli kuwa ninataka kurejea katika ulimwengu wa soka na ninadhani kuwa timu ninayoweza kusajili ni ile niipendayo ya United,” alisema Bolt.
Alisema kuwa watu wanambeza kwa vile hawajabahatika kumuona wakati wa uchezaji wake, lakini anajiamini kuwa anaweza na kama itatokea Kocha wa United, Alex Ferguson, akamuona hawezi akasita kumsajili.
“Ninamaanisha ninachokisema nadhani kama Kocha Alex Ferguson ataniona ataamini kuwa nitakuwa mrithi wa winga wake mahiri Ryan Giggs,” alisema Bolt.
Kwa mujibu wa mwandishi wa gazeti la Guardian, Simon Hattenstone, aliyefanya mazungumzo na Bolt, mwanariadha huyo nyota duniani, ameonyesha dalili za kumaanisha anachokisema.
“Wakati tukizungumza, alinionyesha jinsi alivyozitembelea klabu kuwa za Manchester United na baadaye Bayern Munich ya Ujerumani, ambako alifanya mazoezi na wachezaji wa timu hiyo,” alisema Hattenstone.
Mwanariadha huyo alikuwa amebeba magazeti kadhaa ya michezo, likiwemo la L'Equipe, ambalo lilikuwa na picha zake wakati akifanya mazoezi na Munich na akizungumza na kocha wa timu hiyo Louis van Gaal na pia picha nyingine akishikana mikona na nyota wa timu hiyo Miroslav Klose.

Comments