'TWENDE' DIAMOND JUBILEE KESHO

MAONYESHO maalum yanayohusisha kazi zinazofanywa na wanawake wajasiliamali yajulikanayo kama Tanzania Women Enterpreneurs & Networking Development Exposition ‘TWENDE’ yanatarajiwa kuanza leo katika ukumbi wa Diamond jubille jijini Dar es Salaam.

Mwandaaji wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali alisema kuwa maonyesho hayo yatakayofanyika leo na kesho yataambatana na warsha sambamba na kubadilishana ujuzi miongoni mwa washiriki.
Alisema lengo la maonyesho hayo ni kuendeleza na kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya Taifa kwa kutambua uwezo na mafanikio ya wanawake wajasiriamali, pamoja na wale wenye ulemavu ili kuleta ajira.
Aliongeza kuwa warsha hiyo pia inalenga kuonyesha wanawake wajasiriamali kama mfano wa kuigwa, kuongeza juhudi zao, kutoa ujumbe na kubadilishana mbinu nzuri za kibiashara.
“Pia kuwajenga wafanyabiashara wanawake kwa kuanzisha TWENDE SACCOS, kuendeleza uzalendo wa kutumia bidhaa za Tanzania, kutengeneza jukwaa kwa ajili ya wanawake wenye uwezo mdogo, wa kati, mkubwa na wale wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) kuweza kuonyesha bidhaa na huduma na huduma zao kwa pamoja kwenye mpangilio mzuri”, Alisema.

Comments