TUSKER PROJECT FAME 2010 YAZINDULIWA RASMI

MENEJA MKUU WA UHUSIANO, MAWASILIANO YA JAMII WA SBL, TEDDY MAPUNDA AKIZUNGUMZA KATIKA UZINDUZI WA SHINDANO LA TUSKER PROJECT FAME ULIOFANYIKA LEO KWENYE HOTELI YA MOVENPICK.

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji chake cha Tusker Lager, imezindua rasmi mashindano ya Tusker Project Fame 4 ambapo mshindi atajinyakulia sh. milioni 95 pamoja na kurekodi nyimbo katika studio nchini Afrika Kusini.Mashindano hayo ambayo yanashirikisha nchi za Uganda, Kenya, Tanzania na Rwanda na kuiongeza nchi ya Sudan ya Kusini kwa hapa nchini yatagharimu kiasi cha sh. milioni 300 ambapo wasanii watatu tu wataiwakilisha nchi katika Academy itakayokuwa Kenya.

Comments