TIP TOP KUZINDUA 'BADO TUNAPANDA' SUNSIRO IDD MOSI, KEYSHA ASIMAMISHWA

BABU TALE, MENEJA WA TIP TOP CONNECTION

NYOTA WA TIP TOP, MADEE, DESSO, KEYSHA NA CASSIM

KUNDI maarufu la bongo fleva nchini  Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese litazindua albamu yake ya pamoja 'BADO TUNAPANDA' siku ya EID EL FITR, uzinduzi utakaofanyika katika club ya SUNSIRO.
Meneja wa kundi hilo BABU TALE amesema kwamba uzinduzi huo utapambwa na wasanii kama Linah, Mwasiti, Jaffaray, Roma, Godzila na wengineo.
Kundi hilo lililojizolea umaarufu mkubwa linaundwa na wasanii wanaofanya vema katika medani ya bongo fleva wakiwemo Madee, Tundaman, Cassim, Desso na Keysha.
Hata hivyo,first lady wa kundi hilo Khadija Shaban 'Keysha' hatoshiriki katika uzinduzi huo kutokana na kusimamishwa baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu.

Comments

  1. jamani Keysha au wamemuonea! msameheni basi atajirekebisha jama!!!

    ReplyDelete

Post a Comment