SOKA MAREKANI KUITANGAZA TANZANIA

RAIS WA SOCCER, PATRICK STEENBERGE

CHUO Kikuu cha Drake cha Marekani na Chuo cha CONADEIP cha Mexico wanatarajiwa kutangaza mpira wa Marekani Mei mwakani utakaofahamika kama Kilimanjaro Bowl, kwa sababu Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye maeneo ya kihistoria na utalii.

Rais wa Global Soccer, Patrick Steenberge, amesema leo kuwa  Mei 17, 2011 kutakuwa na matukio mawili likiwemo la kliniki ya mchezo huo itakayofanyika mkoani Kilimanjaro na kuzuru zaidi ya robo ya vivutio vya kitalii ikiwamo Mlima Kilimanjaro.
Steenberge alisema Mei 21 timu za vyuo hivyo zitamenyana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Stadi za Biashara (MUCCOB’s), kabla ya kutembelea vituo vya yatima.
Naye Kaimu Ofisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi, alisema ujio wa timu hizo utaitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya michezo na utalii.

Comments