SHEAR CHARITY BALL 2010 KUFANYIKA OKTOBA 2

MRATIBU WA SHEAR CHARITY BALL, SUZAN MISEDA KULIA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI HAWAPO PICHANI, KUSHOTO NI MWAKILISHI TOKA KITUO CHA WATOTO SOS.

WADAU TOKA SHEAR ILLUSION.

MSANII mahiri wa muziki wa Salsa kutoka nchini Ireland Joush Tasia Rhumba anatarajia kutoa burudani katika hafla maalum ya kuchangia fedha kwa watu wasiojiweza ‘Blast from the past Shear Charity Ball 2010’ itakayofanyika Oktoba 2 kwenye hoteli ya Double Tree by Hilton, iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ambayo imeandaliwa na taasisi ya Shear Illusions itaambatana pia na uzinduzi wa jarida la ‘Shear Hair and Beauty Magazine’ lililopo sokoni kwa mwaka mmoja sasa ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa msaidizi wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanszania, January Makamba.
Msemaji wa hafla hiyo, Suzan Miseda alisema kwamba kupitia tamasha hilo la hisani litakuwa likifanyika kila mwaka ili kutambua mchango wa kuaminika wa wateja wa jarida hilo na kuwahamasisha wateja wapya kuhusu kujiunga na familia ya Shear.
Alisema mapato yatakayopatikana katika tukio hilo yataelekezwa katuika mfuko wa taasisi ya CCBRT ambao hutunisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawakwe wenye ulemavu, ukijikita zaidi kwenye tatizo la fistula ambalo wanawake wanaosumbuliwa nalo na hufanyiwa upasuaji bure katika taasisi hiyo.
“sehemu nyingine ya mapato hayo yatakwenda kwa ‘SOS Children’s Village’, kusaidia maisha watoto yatima na waliotelekezwa ambao hulelewa katika kituo hicho kinacholea watoto wakiwa katika makazi maalum yaliyo kama kijiji”, Alisema.
Aidha, Suzan alisema kwamba ili kuweza kushiriki katika hafla hiyo kutakluwa na tiketi maalum zitakazouzwa kwa shilingi 150, 000 kwa klila meza, huku tamasha hilo likibeba ujumbe wa ‘60’s, 70’s na 80’s ambapo wageni wote watatakiwa kuvaa magauni mazuri yatakayoendana na ujumbe huo.
Imedhaminiwa na  Vodacom Foundation, Benki ya NBC, Chuo cha Pure Academy, Benchmark Productions, Darling, NSSF, Advertising Dar, Sam’s Super Store Ltd, Moss & Plants, Tinamaria Boutique, Clouds Tv & radio, Colosseum Hotel, S.S. Concrete Company Ltd, CCBRT, Shear Illusions, I- View Media, Paradise City Hotel na Double Tree by Hilton Hotel.

Comments