SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO YAFANYIKA LEO



MGENI RASMI KATIKA SEMINA HIYO NAIBU WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO JOEL BENDERA MWENYE SUTI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO, MWENYE SHATI LA DRAFI NI MMOJA YA WAKUFUNZI KATIKA SEMINA HIYO, DAMAS NDUMBARO, WAKALA WA WACHEZAJI ANAYETAMBULIWA NA FIFA.


BENDRA AKIMKABIDHI MWENYEKITI WA TASWA JUMA PINTO KITABU KINACHOHUSU SHERIA NA MIONGOZO YA SOKA, KULIA NI KATIBU MSAIDIZI WA TASWA, GEORGE JOHN.


HAWA BADALA YA KUSIKILIZA SEMINA WANAJIPOZA NA SAYONA, HAO NI SOMOE (NIPASHE), SOFIA (UHURU)NA MWANI (THE AFRICAN)

KILUMANGA (MAGIC FM), KAMBILI (CHAMPION).

CECY (UHURU FM), KHADIJA(WWW.BONGOWEEKEND.BLOGSPOT/TANZANIA DAIMA), KAPINGA (JAMBO LEO)

Mkufunzi mwingine katika semina hiyo, Damas Ndumbaro ambaye ni mwanasheria na pia ni wakala wa wachezaji anayetambulika FiFa aliwataka waandishi wa habari za michezo kufuata sheria za uandishi wa habari kwa kuandika mambo yaliyosahihi na si habari za kutunga.




Mmoja ya wakufunzi hao, Salim Said ambaye ni mwandishi mkongwe aliwataka waandishi wa habari kufuata maadili ya kazi zao ikiwemo suala la mavazi huku akitolea mfano wa kuwahi kuwafukuza wanahabari wawili wa kike toka chuo kimoja alichokuwa akifundisha kutokana na kuvaa mavazi yasiyo na staha.

"Mwandishi uvae mavazi yanayoendana na mazingira, sio unaenda kumuhoji padri unavaa kanzu, au unaenda kijijini unavaa suti...vaeni mavazi ya heshima ambayo hata ukishtukizwa ghafla kwenda mahala unaweza ukaingia nayo.

FRANK SANGA, mhariri wa gazeti la mwanaspoti naye akitoa mada katika semina hiyo.


CLARA, VICKY (MWANANCHI)

MWALI (MAJIARA), FATMA (UHURU FM), ZAINAB (TIMES FM)

BENNY KISAKA (MMOJA YA WAKURUGENZI JAMBO LEO)

MKANDEMBA (SAYARI), JESCA NANGAWE (MWANANCHI)

WAANDISHI wa habari za michezo toka vyombo mbalimbali vya habari leo wamehudhuria semina kuhusiana na masuala mbalimbali ya michezo iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) na kufanyika katika ukumbi wa manispaa ya Temeke.
Katika semina hiyo wakufunzi walitoa mafunzo mbalimbali kwa waandishi hao na hasa changamoto wanazokutana nazo katika kazi zao.
Semina hiyo itaendelea tena kesho.

Comments