RIADHA DAR KUADHIMISHA MIAKA 11 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA

BABA WA TAIFA, MWALIM JK NYERERE

CHAMA cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAAA), kimeandaa mbio maalumu kuadhimisha miaka 11 ya kifo cha baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitakazofanyika Oktoba 14 maeneo ya uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa DAAA, Kapteni mstaafu Lucas Nkungu alisema, mashindano hayo yatakuwa ya Kilomita 6 na 12 kwa wanawake na wanaume.
Nkungu alisema, DAAA itatoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tano, ambao kila mmoja atapatiwa vifaa vya mchezo huo.
Aidha, Nkungu alitoa wito kwa wadau wa michezo nchini, kujitokeza kufanikisha mbio hizo ambazo zitashirikisha klabu za mchezo huo za Mkoa wa Dar es Salaam.
Nkungu alisema, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Mujaya Suleiman Nyambui.

Comments