REDIO TIMES YAWAPIGA JEKI WASANII MAFIA

MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO WA REDIO TIMES, SCOLASTICA MAZULA AKIFAFANUA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI LEO.

KITUO cha redio cha 100.5 Times Fm kimetoa msaaada wa seti ya ngoma na tiksheti kwa kitundi cha sanaa cha Mafia Youth Development cha mjini Mafia ili kiweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi.
HAWA NI WAWAKILISHI WA KIKUNDI HICHO

HAPA SCOLA AKIZIJARIOBU KABLA YA KUWAKABIDHI

Akizungumza katika hafla iliyofanyika katika ofisi za redio hiyo zilizopo Mikocheni,jijini Dar es Salaam mkuu wa kitengo cha Uhusiano wa redio hiyo Scolastika Mazula alisema msaada huo  ni sehemu yao ya kukuza na kuendeleza sanaa za aina mbalimbali.
WAKIKABIDHIWA
Alisema kikundi hicho chenye wasanii 30 kinajihusisha na kuelimisha jamii kwa njia ya sanaa katika mambo mbalimbali ikiwemo Ukimwi, kupiga vita mauaji ya Albino, madawa ya kulevya na mambo mengine.

Comments

  1. nawapa hongera radio time kwa kujiboresha zaidi lakini mmetuambia radio inamitambo ya kisasa mbona hiyo mixer kwa nchi niliyopo ni model ambazo walikuwa wanatumia zamani zana hiyo siyo digital ni analogy digital hazina gage kama hivyo

    ReplyDelete

Post a Comment