PRODUCER/MTANGAZAJI KIDBWAY HALI YAKE YAANZA KURIDHISHA

HALI ya mtangazji wa redio free afica ya Mwanza ambaye pia ni mtayarrishaji wa muziki akimiliki studio za Tetemesha Sandhu Mpanda maarufu kama Kid bway ambaye alip[oteza fahamu tangu jumnanne ya wiki hii baada ya kupigwa na msanii inaridhisha kiasi baada ya kuzinduka na kuanza kutambua ndugu zake.
Kidbway aliyelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando, Mwanza baada ya uchunguzi wa madaktari ilibainika kwamba fuvu lake eneo la nyuma limepasuka hivyo kusababisha  damu kuvujia katika ubongo na nyingine katika uti wa mgongo.
Kwa mantiki hiyo madaktari wanaendelea na matibabu.
Tunamuombea kwa mwenyezi mungu apone haraka aweze kuendelea na shughuli zake.

Comments