'NIPENI MIAKA MINGINE MITANO'


ZAHANATI HII IPO KATIKA MOJA YA MAENEO HAPA NCHINI KWETU AMBAPO WAGONJWA NDIO KAMA UNAVYOWAONA WAKIWA WAMELAZWAZWA WODINI.

Ndugu wananchi wapendwa..haki ya nani niongezeeni miaka mingine mitano.ili niendeleze kasi ya maendeleo katika jimbo langu la mjomba..nguvu bado zimejaa tele...!! na kasi ya safari hii, mithili ya vigogo wa world kapu wanavyo ondolewa ktk mashindano..naapa nitapaaza sauti kushinda mavuvuzela katika kuwaletea zahanati za kisasa zaidi kuliko hii.ambayo kama mnavyo ona wafadhili walinipa vitanda vyenye internet. na drip zenye bia yetu pendwa ya safari..aidha waganga na wahudumu wote nita wapeleka refresher kozi kwa toboa tobo..ktk jiji la bwagamoyo.

Nanyi mnae nionea gere mjomba... dawa yenu ipo.nita wafungulia bendi ya fm segerea.a.k.a ukonga sound,a.k.a keko vibration ehee..ndio,mnashangaa nini.na kwa wale mashabiki wangu mjomba sijawatupa.safari hii nimewaombea jezi za timu ya weldi kapu ya mzee madiba,..ndio..siwenyewe mnaziona rangi zetuuu..kwa kifupi miaka mitano hii ninayo iomba mjomba!! nikuhakikisha vile viji miradi vyote navikamilisha bwana!!! basi niwaage kwa kuwaombea usingizi mzito hadi hapo kamjomba nako katakapo kuwa kana tangaza nia kugombea jimbo letu 2015. wasalaam mjomba.
NIMETUMIWA NA JAMES BIBOZE.

Comments