NIMEIPENDA HII STYLE YA KUJIKINGA NA MBU





JANA usiku nilipokuwa katika kiwanda cha uchapaji cha Printech kilichopo barabara ya Morogoro eneo la Shekilango nilivutiwa na mmoja ya wafanyakazi kwa jinsi alivyoamua kujilinda dhidi ya mbu ambao wanaambukiza Malaria.
Kama unavyojua kazi ya magazeti hufanywa usiku na mchana hivyo kutokana na mida hiyo ya usiku mbu kuwa wengi yeye aliamua kujilinda nao kwa kufunga karatasi nene katika miguu yake.
Nadhani kama kila mmoja wetu angetumia njia nmyingine mbadala kwa ajili ya kujikinga na mbu, maambukizi ya ugonjwa huu yangepungua.

Comments