MSONDO NGOMA KUVAMIA MIKOA YA KUSINI

BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma imeondoka jijini Dar es Salaam kwa ziara ya maonesho matano katika mikoa ya kusini kuanzia Oktoba mosi mwaka huu, baada ya kukaa muda mrefu bila kutembelea kanda hiyo.
Akizungumza jijini Dar leo, Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' (pichani)amesema kuwa ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuitamulisha albamu yao mpya ya Huna Shukrani.
"Tukiwa huko tutafanya kazi ya kuwapa burudani na wapenzi wetu watapata nafasi ya kuona mambo mengi yanayohusu bendi yao kama hayo niliyoyasema.," alisema Mhamila.
Amesema kuwa wataanzia kuangusha burudani ya aian yake katika ukumbi wa Bwalo la Maendeleo, Kilwa na Hoteli ya Lindi Oktoba mosi, ambapo oktoba 2 watakuwa Brantare Hall na oktoba 3 watakuwa katika ukumbi wa Madeko Masasi, Oktoba 4 Nachingwea na 5 watakuwa Nyongoro Hall, Ruangwa.
Mhamila amesema kuwa mbali na utambulisho wa albamu hiyo, bendi hiyo pia itatoa fursa kwa wapenzi wake wa mikoa hiyo kwa lengo la kusikilizishwa vibao vipya ikiwemo Dawa ya deni kulipa na Lipi Jema vilivyoimbwa na wasanii mahiri akiwamo Edo Sanga.

Comments