MSONDO NGOMA KUKAMUA TCC CLUB, CHANG'OMBE EID MOSI

                             
Bendi kongwe nchini, Msondo Ngoma , inatarajia kuwapagawisha mashabiki wa muziki wa dansi siku ya Idd Mosi kwenye bonanza maalum litakayofanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang’ombe.
Bonanza hilo ambalo limepangwa kuanza saa 11 jioni, limeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi.
Mratibu wa bonanza hilo Joseph Kapinga amesema kuwa Msondo Ngoma itatumia onyesho hilo kupromoti albamu yao mpya ijulikanayo kama Huna Shuktani kabla bendi haijasafiri kwenda Zanzibar siku ya Iddi pili kwa maonyesho mengine zaidi.
Albamu hiyo ina nyimbo zingine kama Huna Shukrani ambayo imetungwa na Saidi Mabera, Cheo ni Dhamana (Eddo Sanga), Kiapo (Hussein Jumbe), Mama Kosi (Joseph Maina), Machimbo (DJ Papa Upanga) na Haki Yangu Iko Wapi (H. Huvuruge).
Pia wapenzi wao wataburudika na nyimbo zao za zamani kana Kilio Cha Mtu Mzima, Kaza Moyo, Piga Ua Talaka Utatoa na mengineyo. Pia Zawadi mbalimbali zitatolewa na Konyagi.

Comments