MAONYESHO YA 'TWENDE' YAMALIZIKA KWA WASHIRIKI KUPATA MAFANIKIO

US AMBASSADOR ALFONSO LENHARDT LISTENING TO CONTRIBUTIONS OF WOMEN ENTERPRENEWESHIP
AMBASSADOR ALFONSO LOOKING A BATIK SHIRT MAKING BY FARHA SULTAN

MS TERESIA MISTRY FROM ZANZIBAR DISCUSSING WITH AMBASSADOR ALFONSO

TANZANIAN WOMEN ENTEPRENEURS AS THEY LISTEN TO THE AMBASSADOR'S SPEECH

Wanawake wajasiriamali wa Tanzania wajitokiwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika jukwaa la TWENDE, jukwaa lililotoa fursa kwa wanawake wajasariamali kuweze kuuza, kuonyesha na kutambulisha kazi zao kwa ufasaha kwa jamii ya watanzania.
Kauli hiyo imetolewa na wanawake wajasiriamali ambao wameshiriki katika jukwaa la (TWENDE) Tanzania Women Entrepreneurs & Networking Development) lilodumu kwa sikumbili katika ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 16 na 17 ya mwezi huu jijini Dar es salaam walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari katika 361 degrees Kinondoni kinondoni jijini Dar es salaam.
Wanawake hao wamesema fursa kama hii ya jukwaa la TWENDE ni muhimu na zinahitajika zaidi kwa wanawake wajasirimali kwani zinawawezesha kujitangaza, kuuza pamoja na kubadilishana mawazo yanayosaidia kukuza nyanja ya ujasiriamali kwa ujumla.
“Kupitia jukwaa la TWENDE tumeweza kujitangaza na watanzania kufahamu wanawake wajasirimali wa Tanzania wapo wapi na wanafanya nini, ni fursa muhimu na ya kipekee kwetu sisi kama wanawake”. Amesema Stella Kibonde.
Aidha wanawake hao wamesema umefika wakati sasa kwa wanawake wajasariamali Tanzania kufanya biashara za aina tofauti ili kuweza kuleta ushindani zaidi kibiashara. Pamoja na hayo pia wanawake hao wametoa wito kwa watanzania kupenda na kuthamini bidhaa zinazozalishwa na wanawake wajasirimali wa hapa nchini.
“Watanzania wapende kununua bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali na zinazozalishwa hapa nchini, kwani zina nbora unaokubalika, kwa kufanya hivyo watakuwa wamechangia pato la masariliamali na hata taifa kwa ujumla” alisema Shamsa Hamud.
TWENDE ni jukwaa la wanawake wajasiriamali Tanzania , huu ni mwaka wake wa kwanza na litakuwa likifanyika kila mwaka na kuwahusisha wanawake wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar .
Tanzania Women Entrepreneurs & Networking Development Exposition imepanga kuleta maendeleo ya wanawake kwani ni jukwaa mahususi limewakutanisha wanawake wajasiriamli wa Tanzania zaidi ya 100 na dhumuni la TWENDE ni kuthamini na kutambua mchango wa wanawake wajasiriamali kwa maendeleo ya Taifa.

Comments