MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE YA JITEGEMEE SEKONDARI

Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi Mwanafunzi Mwanahawa Amiry cheti pamoja na zawadi kwa kufanya vizuri katika kipaji cha kucheza ngoma za asili katika shule ya JKT Jitegemee kwenye mahafali ya 26 ya kidato cha nne yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo, katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Raymond Mpazi.


Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akifurahia jambo pamoja na Mwanafunzi wa JKT Jitegemee Imani Gwasa wakati akimkabidhi cheti cha mwanafunzi bora wa somo la kemia shuleni hapo kwenye mahafali ya 26 ya kidato cha nne yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.


Mkurugenzi wa Mahusiano wa  Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi  Mwanafunzi Anyelwisye Mwakibinga  cheti cha kutambuliwa kama kiongozi bora wa Scout katika shule ya JKT Jitegemee kwenye  mahafali ya 26 ya kidato cha nne shuleni hapo, wanaoshuhudia  kulia ni Kaimu Mkuu  wa shule hiyo Meja  Michael Mtenjele na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule  Raymond  Mpazi
Baadhi ya wanafunzi  wavulana wa JKT Jitegemee wa kidato cha Nne walioshiriki katika mahafali ya 26 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.

Baadhi ya wanafunzi  wasichana  wa JKT Jitegemee wa kidato cha Nne walioshiriki katika mahafali ya 26 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.

Comments