KUZINA YANGA, FC LEOPARDS 10,000 na 3,000

KIKOSI CHA YANGA

KIKOSI CHA AFC LEOPARDS

KIINGILIO cha juu katika mechi ya kimataifa ya kirafiki katika AFC Leopards ya Kenya na Yanga itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha kimepangwa kuwa shilingi 10, 000 kwa jukwaa kuu na 3,000 mzunguko.
Akizungumza kwa njia ya simu leo na kutoka Arusha mratibu wa mechi hiyo, George Wakuganda alisema kwamba maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo yanakwenda vizuri na kwamba timu zote zinatarajiwa kuwasili huko kesho.
Alisema mechi hiyo ni maalum kwa kuipa makali Yanga kabla ya mechi yake ya Ligi Kuu ya Vodacom na AFC ya Arusha inayotarajiwa kupigwa jumamosi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Aliongeza kuwa kupitia mechi hiyo kocha wa Yanga Kostadin Papic ataangalia mapungufu yatakayojitokeza kaytika kikosi chake ili kuweza kuyafanyia marekebisho kabla ya mechi yao na AFC.
“Tunaomba mashabiki wa soka wa nmkoa wa Arusha klujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo ili kuweza kuona vipaji vya wachezaji wa timu zote, kwani tumeamua kuwapa heshima wakazio wa huko kwa kuwaletea mechi hii”,Alisema Wakuganda.

Comments