JARIDA LA MAN LATAMBULISHWA RASMI

MTENDAJI mkuu wa kampuni ya Euro Cosultancy Limited inayochapisha jarida la Man, Dismas Masawe katikati akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa hafla ya utambulisho wa jarida hilo jana kwenyec hoteli ya New Africa, kushoto ni mmoja ya wadau wa jarida hilo, Brett Dean Frances na kulia ni mhariri mkuu wa jarida hilo, Taji Liundi.





MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO WA GAZETI LA NIPASHE SOMOE NG'ITU AKIULIZA SWALI KUHUSIANA NA JARIDA HILO.
JARIDA maalum linaloandika habari za wanaume lijulikanalo kama ‘Man’ limetambulishwa rasmi leo kupitia hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa, jijini Dar es Salaam.

Mtendaji mkuu wa kampuni ya Euro Consultancy Limited inayochapisha jarida hilo, Dismas Masawe alisema kwamba wameamua kuanzisha jarida hilo kutokana na majarida mengi yaliyopo kuandika zaidi habari za wanawake.
Alisema kutokana na uwepo wa jarida hilo Wanaume wa Kitanzania sasa watakuwa wanajivunia huku jarida hilo litakuwa likigusa mambo yao mbalimbali ikiwemo afya, biashara, michezo na maisha ya kawaida.
Aliongeza kuwa jadida hilo litakuwa likichambua mambo mbalimbali ambayo msomaji angependa kuyajua kuanzia mambo ya magari, ujenzi, taasiisi za fedha, masuala ya uchukuzi, michezo, teknolojia, mitindo, uhusiano na kupitia mambo mengine yanayoizunguika jamii.
Tayari jarida hilo linalotoka kila baada ya miezi miwili limeshatoa matoleo manne na ndani ya matoleo hayo wanawake wanaweza kutumia kama jukwaa la kuwatambua wanaume.
Jarida hilo linauxzwa kwa fedha za kitabnzania shilingi 5,000 na linapatikana kote nchini.

Comments

  1. jamani somoe nakupenda na rafiki yako sophia lakini lile bonge lenu mbayaaaaaaaaaaa jeupe kama papai mbayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete

Post a Comment