JANE MISSO KUZINDUA ALBAMU SEPTEMBA 19

JANE MISSO KATIKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO KUSHOTO NI GODFREY KATULA AMBAYE NI MWENYEKITI WA KATI YA MAANDALIZI NA KULIA NI HUMPHREY MAZIBA

MSANII wa muziki wa Injili nchini Jane Misso anatarajia kuzindua albamu yake ijulikanayo kama ‘Uinuliwe’, Septemba 19 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jane alisema maandalizi yanakwenda vizuri na uzinduzi huo utapambwa na wasanii toka ndani na nje ya nchi.
Alisema albamu hiyo iliyosheheni nyimbo zenye ujumbe wa kuombea amani katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 11 mwaka huu.
Aliongeza kuwa albamu hiyo inaundwa na nyimbo sita zikiwemo ‘Uinuliwe’ ambao umebeba jina la albamu, ‘Motema’, ‘Pokea Sifa’, Nyosha Mkono Wako’, ‘Unaweza Yote’ na ‘Mimi Najua Neno Moja’.
Aidha uzinduzi huo utaambata pia na uzinduzi wa albamu ya video za albamu hiyo ambayo imetayarishwa na kampuni ya Haak Neel Production (T) LTD.

mwisho

Comments