HASSANALI KUWAPA MAFUNZO YA SIKU MBILI WANAWAKE WAJASIRIAMALI

Wanawake wajasiriamali zaidi ya 100 kutoka maeneo tofauti ya Tanzania watajumuika pamoja katika jukwaa linalojulikana kwa lina la TWENDE, ikiwa na maana ya(Tanzania Women Entrepreneurs Networking & Development Expositions). Jukwaa litafanyika tarehe 16 na 17 Septemba ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam .
“TWENDE ni jukwaa la siku mbili la wajasiriamali wanawake linatoa fursa ya kuuza na kuonyesha bidhaa mbalimbali wanazozalisha. Ni jukwaa likalo wakutanisha wanawake wajasiriamli wanaomiliki na kufanya biashara za aina tofauti, wale wa kubwa, wa kati na hata wafanyabiasrawa wadogo, pamoja na taasisi za kiserikali na zile zisizo za kiserikali. Sambamba na hilo , pia watapata nafasi ya kushiriki katika semina itakayokwenda sambamba na jukwaa hilo ambayo imelenga kuelimisha na kuwawezesha wanawake wajasiriamali.
Lengo kuu la kuandaa TWENDE ni kuendeleza na kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa kwa kutambua uwezo wao na mafanikio ya wajasiriamali wanawake, ukijumisha na wale wenye ulemavu ili kuleta ajira na maendeleo kwa wote. Pia ni kuonesha wajasiriamali wanawake kama mfano wa kuigwa, kuongeza juhudi za maendeleo ya wanawake wajasiriamali, kutoa ujumbe na kubadilishana mbinu mbalimbali za kibiashara, kuendeleza uzalendo wa kutumia bidhaa zinazotengenezwa na watanzania. TWENDE ni jukwaa litakalo kuwa likifanyika kila mwaka ambalo litakuwa linaandaliwa kitaalam zaidi na kuwawezesha wanawake kuuza na kuonyesha bidhaa zao pamoja
“Wanawamake ni wajasiriamali kwa kuzaliwa, wanachohitaji ni kupata nafasi mbalimbali zitakazokuza vipaji vyao kibiashara, ndio maana nikaona nianze na TWENDE kwa lengo la kuwezesha wanaweke wajasiriamali kukutana pamoja na kuwawezesha kupata mbinu mbalimbali za kuweza kujipatia kipato cha kila siku kupitia biashara wanazozalisha”. Alisema Mustafa Hassanali mwanzilishi wa TWENDE
Tanzania Women Entrepreneurs Networking and Development Exposition ni jukwaa litakalowaleta wanawake wajasiriamali na wanaharakati wa Tanzania pamoja. Ni jukwaa litajumuisha uuzaji wa bidhaa, huduma na maonesho kwa ujumla, sambamba na warsha ambayo itawawezesha wajasiriamli kujifunza mbinu mbalimbali za mafanikio kutoka kwa wanawake waliofanikiwa kibiashara na kutoa mchango mkubwa kwa jamii.
“TWENDE imepanga kuleta maendeleo ya wanawake kwa kuandaa tukio ambalo litawakutanisha pamoja wanawake wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani ili waweze kuonesha kazi zao, kujitangaza na kuuza bidhaa zao. Sambamba na semina ya siku mbili itakayotoa elimu bora juu ya maswala ya kibiashara kwa wajasiriamali watakaoshiriki”, Alifafanua Mustafa.
TWENDE (Tanzania Women Entrepreneurs Network & Development Exposition) imedhaminiwa na 361 Degrees, Delfina, Global Outdoor Media and United States of America Embassy in Dar es Salaam .

Saphia Ngalapi
Media & PR Manager
Mustafa Hassanali

Comments