HAFSA KAZINJA AIBUKIA FM ACADEMIA KUTAMBULISHWA DIAMOND JUBILEE IDD EL FITR

HAFSA KAZINJA KITAKATI AKIWAIMBIA KIDOGO WAANDISHI WA HABARI HAWAPO PICHANI.\

RAIS WA FM ACADEMIA NYOSHI EL SAADAT KUSHOTO NA MENEJA UHUSIANO WA KAMPUNUI ZA SIMU ZA MKONONI ZAIN, MUGANYIZI MUTA.

ALIYESHIKA CHUPA YA HEINEKEN NI MENEJA WA KAMPUNI YA MABIBO BEER INAYOIZALISHA jEROME RUGEMALILA AKIONYESHA CHUPA MPYA YA BIA HIYO YENYE UJAZO WA 25 CL AMBAYO ITAZINDULIWA SAMBAM,ABA NA ALBAMU YA VUTA NIKUVUTE.

BAADHI YA WANAMUZIKI WA FM ACADEMIA.

WAKIIMBA FREE STYLE KWA WAANDISHI WA HABARI

MSANII wa kizazi kipya anayepiga katika mtindo wa Zouk, Hafsa Kazinja amejinunga na bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia na atatambulishwa rasmi siku ya uzinduzi wa albamu mpya ya bendi hiyo ijulikanayo kama ‘Vuta Nikuvute’ utakaofanyika siku ya Eid Moso kwenye ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo kwenye ukumbi wa Triz Motel, rais wa bendi hiyo Nyoshi El Sadat alisema msanii huyo anaendelea na mazoezi kwa ajili ya uzinduzi wa bendi hiyo yanayofanyika katika ukumbi huo.
Alisema maandalizi kwa ajili ya uzinduzi wa albamu hiyo yenye nyimbo 15 yanaenda vema ambapo pi a utaambatana na uzinduzi wa chupa mpya ya kinywaji cha Heineken chenye ujazo wa 25 cl, hivyo kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo.
Alizitaja nyimbo zitakazokuwemo katika albamu hiyo ni pamoha na Heshima kwa Wanawake, Vuta Nikuvute, Mwili Wangu, Jasmine, Moize Katumbi, Fadhila kwa Mzazi, Siku ya Jumatano, Matatizo Yangu, Mgeni, Rumba, Vuta Nikuvute Remix, Heineken Ngwasuma na Introduction.
Aidha uzinduzi huo ambao umedhanminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain pamoja na kampuni ya Mabibo Beer inayozalisha bia ya Heineken utasindikizwa na msanii kutoka Kenya, Nameless.

Comments