GENEVIEV EMMANUEL MPANGALA - VODACOM MISS TZ 2010/2011

VODACOM MISS TANZANIA 2010/2011 GENEVIEV MPANGALA KATIKATI MARA BAADA YA KUTWAA TAJI HILO SEPTEMBA 11 KATIKA SHINDANO LILILOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY, JIJINI DAR ES SALAAM.


TANO BORA.

GENEVIEV alitwaa taji hilo baada ya kuwapiku wenzake 29 alizawadiwa gari aina ya Hyundai i 10 lenye thamani ya shilingi milioni 12 pamoja na fedha taslimu shilingi milioni 10.

KUMI BORA.
kabla ya ushindi huo, Geneviev ambaye ni mtoto wa meneja wa timu ya soka Yanga, Emmanuel Mpangala, alikuwa anashikilia taji la Miss Temeke na lile la Miss Chang'ombe.

Nafasi ya pili  ilikwenda kwa Gloria Mwanga ambaye alizawadiwa milioni 6.2, huku mshindi wa tatu ikienda kwa Consolata Lukosi aliyezawadiwa milioni 4.Lukos pia alitwaa taji la balozi wa mitindo wa kinywaji cgha Redd's.
Nafasi ya nne ilitwaliwa na Beatrice Premsingh ambaye alipewa milioni tatu, na wa tano alikuwa Pendo Sama aliyeoondoka na milioni 2.4.
Alice Lushiku, Flora Martin, Salma Mwakalukwa, Anna Daudi na Britnie Urassa ambao waliingia kumi bora kila mmoja alipata mil.1.4, huku washiriki wengine waliosalia waliondoka na kifuta jasho cha shilingi 700,000 kila mmoja.

MATAJI MENGINE
-BALOZI WA UTALII-SALMA MWAKALUKWA
-CHUO CHA UREMBO CHA PURE- BRITINIE URASSA
-MULTICHOICE TAJI LA KIPAJI -FLORA FLORENCE
-BALOZI WA REDD'S -CONSOLATA LUKOS

 Shindano hilo li,lipambwa na burudani toka kwa Mheshimiwa Temba na Chegge kutoka kundi la TMK Family, Ambwene Yessayah ‘AY’ , Mataluma, Mwasiti, Lina, Wahu kutoka nchini Kenya na kundi la Tanzania House Of Talent (THT).

Comments