FM ACADEMIA KUKAMUA MBAGALA SEPTEMBA 24


BENDI ya muziki wa dansi ya Fm Academa ‘Wazee wa Ngwasuma’ Septemba 24 inatarajiwa kufanya onyesho la uzinduzi wa albamu yake ya ‘Vuta Nikuvute’ kwa wakazi wa Mbagala na maeneo jirani, onyesho litakalofanyika kwenye ukumbi wa Rawina Resort uliopo Mbagala Kuu.
Mratibu wa onyesho hilo, Zahor Said amesema kwamba onyesho hilo ni kutoa fursa kwa mashabiki wa burudani wa maeneo hayo kupata burudani baada ya kukosa kushuhudia uzinduzi wa albamu hiyo uliofanyioka siku ya Eid Mosi katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni pamoja na Heshima kwa Wanawake, Vuta Nikuvute, Mwili Wangu, Jasmine, Moize Katumbi, Fadhila kwa Mzazi, Siku ya Jumatano, Matatizo Yangu, Mgeni, Rumba, Vuta Nikuvute Remix, Heineken Ngwasuma na Introduction.
Zahor alisema maandalizi yanakwenda vizuri ambapo onyesho hilo litaambatana na utambulisho mwanamuziki wa zouk aliyejiunga na bendi hiyo hivi karibuni Hafsa Kazinja, pia utasindikizwa na vikundi viwili vya unenguaji vinavyotamba katika miondoko ya kiduku.
Aliongeza kuwa onyesho hilo limedhaminiwa na kampuni ya Mabibo wine kupitia bia ya Heineken, Inoch, pamoja na blog za mamapipiro, fullshangwe na janejohn5.

Comments

Post a Comment