FILAMU YA AUNT SUZZY SOKONI



BAADA ya kutamba na filamu ya Fake Pregnant Mwandaaji na Msani nyota nchini anayekuja juu kwa sasa Daud Michael anatalajia kuingiza sokoni filamu yake mpya ijulikanayo kwa jina la ‘Aunt Suzzy’ iliyosheheni mastaa kibao waliobobea kwenye filamu za kibongo.
Akiongea na blog team, leo jijini Dar es Salaam, Daudi ambaye ni mmiliki na Mkurugenzi wa Studio ya D. Production alisema kuwa filamu hiyo inatalajia kuingia sokoni kuanzia sasa na itapatikana kila kona na itakuwa tishio kutokana na jinsi ilivyoigizwa kwa kiwango cha hali ya juu.
“Siku zote mimi nafanya vitu vya uhakika hivyo wadau waisubiri wa hamu filamu ya Aunt Suzzy ambayo itapatikana nchi nzima” alisema Daud.
Daud alisema filamu hiyo ambayo imewashirikisha mastaa mbalimbali wa filamu nchini wakiwemo; Mzee Magari, Daud Michael, Fred Kaguo a.k. mbishi lealy aliyeimba wimbo ‘Tozi wa Mbagala’, Ester FlaviAn, Sara Suddy, Ayubu Santana, Halima Madiwa ‘AUNT Suzzy’ na Diana aliyewika kwenye filamu ya Fake Pregnant.
Aliwataka wadau wa filamu kuisubiria kwa hamu kujionea uondo wa filamu hiyo iliyojaa kila aina ya utaalam kutoka kwa waigizaji hao mahili na wengine wengi huku ukielezea juu ya visa, Mapenzi ya Usaliti, Udhuni na ‘Action’ za hali ya juu.
Filamu hiyo ya Aunt Suzzy inatalajiwa kusambazwa na B4U Entertainment na itapatikana nchi nzima aliwataka

Comments