YES WE CAN! - POULSEN

KOCHA WA STARS JAN POILSEN AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

KOCHA MSAIDIZI WA STARS SYLVESTER MARSH  KUSHOTO NA POULSEN

NAIBU WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO JOEL BENDERA AKIMKABIDHI KAIMU MKUU WA MSAFARA WA STARS MZEE ZAM ALLY.

RAIS WA TFF, LEODGER TENGA AKIFAFANUA JAMBO KWA WAANDISHI WAHABARI, KULIA KWAKE NI BENDERA, NAIBU WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO.








YES we Can!hiyo ni kauli mbiu aliyokuwa akitumia rais wa Marekani Barrack Obama wakati wa kampeni za kuwania urais ambayo leo hii kocha wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mdenmark Jan Poulsen ameitoa akisema wanaweza kuifunga timu ya Algeria.
Stars inatarajiwa kuondoka kesho kwenda nchini Algeria tayari kwa mechi yao ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Africa (CAN) itakayopigwa Septemba tano.
Akizungumza leo katika hafla ya kukiaga kikosi hicho katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam, Poulsen alisema kuwa pamoja na kucheza na timu iliyoshiriki kombe la dunia wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanashinda.
Awali Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera ambaye aliikabidhi bendera timu hiyo aliwataka wachezaji wa timu hiyo kupamba na hatimaye kurejea na ushindi.
Aliwaasa wachezaji hao kujenga ari ya ushindi kinyume na hapo watakuwa wanashindwa kila siku na hiyo inatokana na sababu hawajaamua kushinda.
“Watanzania wamechoka, wanataka ushindi…ushindi hauletwi na TFF, wananchi au wadhamini ila ni ninyi, hivyo mhakikishe mnashinda mechi hiyo…haiwezekani tuwe wasindikizaji kila siku”, Alisema.
Bendera aliongeza kuwa licha ya wachezaji wa timu hiyo kubobea bado hawajawafurahisha watanzania, hivyo amewataka kutumia kila mbinu walizopewa na kocha wao kuhakikisha wanashinda.
Naye rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Leodger Chilla Tenga aliwataka wachezaji hao kutumia uzoefu waliona katika mashindano ya kimataifa ili kuweza kushinda na kuondoka na pointi tatu.
“Tunawafahamu Algeria katiKa soka kuwa ni wazuri, ni mechi ngumu na pia rahisi, ugumu wake ni kuwa wanacheza nyumbani, hivyo ninaamini mtaanza vizuri kwa kuondoka na pointi tatu”, Alisema.
Msafara wa watu 25 wakiwemo wachezaji 20 na viongozi watano utaondoka kesho mchana.

Comments