YATIMA WAANDALIWA BONANZA IDDI PILI


TAASISI ya michezo ya Popular Sports and Entertainment (PSET) ya jijini Dar es Salaam imeandaa bonanza maalum kwa ajili ya watoto yatima wanaoisjhi katika mazingira magumu litakalofanyika siku ya Eid pili katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandisjhi wa habari jana mkurugenzi wa kampuni hiyo Osman Kazi alisema kwamba lengo la bonanza hilo ni kuwathamini na kutoa nafasi kwa watu wenye mapenzi mema kuweza kushirikiana nao katika sikukuu hiyo.
Alisema bonanza hilo ambalo limedhaminiwa na hoteli ya Movenpick litashirikisha watoto zaidi ya 500 kutoka vituo tisa vikiwemo New Life, Umra, Chakuhama, Al Madina, Ilali, Mwandaliwa, Malaika na Dogodogo Centre.
Aliongeza kuwa kupitia bonanza hilo kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo soka, mbio za magunia, kuruka kamba, kutembea, kukimbiza kuku, mbio za vijiko, kupuliza Vuvuzela na michezo mingine ya watoto ambapo washindi watapewa zawadi mbalimbnali.
“Tunawashukuru Movenpick Hotel kwa kusaidia kutoa vinywaji katika tamasha hilo hivyo tunaomba taasisi nyingine na mashirika, na watu binafsio wajitokeze kusaidia ili kufanikisha tamasha hili na kuwafanya walengwa wajisikie kuwa nao jamii inawajali”, Aliongeza.

Comments