YANGA, MTIBWA KUCHEZA MECHI MAALUM YA KUMUAGA MWAKALEBELA J'5


FREDERICK MWAKALEBELA

MECHI ya kirafiki kati ya Yanga na Mtibwa Sugar ya Morogoro itakayochezwa jumatano  kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, itatumika kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela.


Mratibu wa mechi hiyo, Geogee Wakuganda amesema  kuwa, wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kumpa heshima Mwakalebela aliyemaliza muda wake TFF na kugeukia siasa.

Alisema wameamua kuichagua Mtibwa Sugar kwa sababu, Mwakalebela aliwahi kufanya kazi katika kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kinachomiliki timu hiyo.

Wakuganda alisema maandalizi ya mechi hiyo, yanaendelea vema na timu zote zimethibitisha kucheza, hivyo amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Aidha, timu hizo pia zitatumia mechi hiyo kupima uwezo wa vikosi vyao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara itakayoanza Agosti 21.

Siku hiyo Yanga itacheza na Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma huku Mtibwa Sugar ikicheza na Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji.

Comments

  1. huyu ndio kiongozi wa ukweli anayetakiwa kuongoza Tanzania na si Iringa mjini pekee kwa sababu amefanya mengi zaidi.
    big up!

    ReplyDelete
  2. Mwakalebela kuagwa na Mtibwa na Yanga si penyewe inatakiwa iitwe timu kutoka nje ya Tanzania, msimtukane Mwakalebela kwa kimechi hicho

    ReplyDelete

Post a Comment