WASHIRIKI FAINALI MISS TZ 2010 KAMBINI AGOSTI 16


MIRIAM GERALD, MISS TANZANIA ANAYEMALIZA MUDA WAKE

KAMPUNI ya Lino ya Lino International Agency  inayoratibu shindano la Miss Tanzania imetangaza majina ya warembo 31 ambao wataingia kambini kwenye Hoteli ya Giraffe Agosti 16 tayari kwa shindano litakalofanyika Septemba 11 jijini Dar es Salaam.


Taarifa ya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Lino Agency, Hashim Lundenga iliwataja washiriki hao na maeneo wanayotoka kwenye mabano kuwa ni pamoja na  Esther Dennis, Gloria (UDSM),Shadia Mohammed, Furaha David, Mary Kagali (Nyanda za Juu Kusini), Bahati Chando, Salma Mwakalukwa, Consolata Lukosi (Kanda ya Kati),Flora Florence, Mary Adam,  Angelina Ndege (Kanda ya Mashariki), Alice Lushiku, Irene Hezron, Amisuu Malick (Kanda ya Kinondoni), Genevive Emmanuel, Anna Daudi, Britney Urassa (Kanda ya Temeke),

Wengine ni Glory Mwanga, Prisca Mkonyi na Jally Murei (Kanda ya Kaskazini), Gloria Mosha, Christine Justine (Kanda ya Chuo Kikuu Huria), Flora Martin, Rachel Sindbad,  PendoSam (Kanda ya Elimu ya Juu), Fatma Ibrahim, Buduri Ibrahim na Margareth Godson (Kanda ya Ziwa).

Comments