WABUNIFU WA MAVAZI WAPIGWA MSASA

Wabunifu wa mavazi 12 wanapata mafunzo yaliyoandaliwa na Swahili Fashion Week kwa kushirikiana na Tanzania Cotton Board (TCB) na Textile Sector Development Unit (TSDU) yenye lengo la kuboresha taaluma ya ubunifu wa mavazi hapa nchini.
“kwa siku ya kwanza tu nimejifunza mengi, natarajia kupata mengi zaidi katika masula mazima ya kuboresha kazi yangu na jinsi ya kutafuta masoko ya ndani na nje”. Alisema Salim Ally mbunifu wa mavazi anayechipikia katika fani hasa kwa upande wa mavazi ya vijana katika mtindo unaojulikana kama la Mtoko wear.
Miongoni mwa wabunifu waliopata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo ni pamoja na Kemi Kalikawe, Margherita Marvassi kutoka Zanzibar , Jamila Vera Swai, Zamda George, Francisca Shirima, Farha Sultan, Ailinda Sawe, Manju Msita, Salim Ally, Kim Dean, Rabi Morro na Angelo Elly Mlaki.
“Tunaamini kwamba mafunzo haya yatawawezesha wabunifu wa watanzania kuweweza kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo zitaweza kuuzwa sehemu yoyote. Pia kupitia mafunzo haya tunaamini kwamba wabunifu watapata habari muhimu zitakazowawezesha kuchangia moja kwa moja ukuaji wa sekta ya ubunifu Tanzania ”. Alisema Mustafa Hassanali muaandaji wa Swahili Fashion Week.
Mafunzo hayo ya siku nne yanaendeshwa na Claire Hamer-Stubbs ambae anatoka katika kampuni ya Ei8ht (www.ei8ht.org), kundi ambalo limekuwa likifanya kazi zake nchini Uingereza, na yanafanyika katika hoteli ya New Africa.
Textile Sector Development Unit (TSDU) kwa sasa inashirikiana na Swahili Fashion Week katika programu ya kuwasaidia wabunifu wa Tanzania kwa kutoa mafunzo ya awali , TSDU inaamini kwamba kwa kutoa fursa ya mafunzo kwa wabunifu ambayo yatawawezesha kutambua mpangilio mzima wa kufanya kazi zao kwa ubora zaidi. Pia inaamini kwamba kupitia semina hii wabunifu watajipatia uelewa mpana wa kufanya kazi na wanunuzi wa rejareja kutoka Uingereza ambao huenda wakavutiwa na bidhaa zinazozalishwa na wabunifu wa Tanzania .

Comments