VODACOM YAKABIDHI VIFAA KWA TIMU ZA LIGI KUU


MKUU WA UDHAMINI WA VODACOM, GEORGE RWEHUMBIZA


JEZI YA SIMBA
AZAM FC
KAGERA SUGAR
AFRICAN LYON
MTIBWA SUGAR
RUVU SHOOTING
TOTO AFRICAN
YANGA
POLISI DODOMA
MAJIMAJI

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom imetenga zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya kudhamini ligi kuu bara msimu wa 2010/2011 unaotarajiwa kuanza Agosti 21 na kushirikisha timu 12.


Hayo yamesemwa leo na meneja udhamini wa Vodacom George Rwehumbiza katika hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vitakavyotumika katika ligi hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa DICC.

Rwehumbiza alisema katika fedha hizo shilingi milioni 667 zimetengwa kwa shughuli za uendeshaji wa ligi hiyo ikiwemo nauli za timu na gharama nyingine ikiwemo posho za waamuzi.

Vifaa vilivyotolewa kwa timu shiriki vina thamani ya shilingi mil.290 ambapo Rwehumbiza alivitaka vilabu hivyo kuvitumia kama chanamoto ya kufanya vizuri katika ligi hiyo na hivyo kupata wawakilishi bora katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Timu zitakazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na mabingwa watetezi Simba, Yanga, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, African Lyon, AFC, Azam, Polisi Dodoma, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Majimaji na Toto African.

Comments