VODACOM MISS TANZANIA WATEMBELEA MONDULI

Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Wasichana Maasai iliyopo Monduli Mkoani Arusha wakati wa rembo hao walipotembelea shule hiyo jana wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Mkurugenzi wa Lino Interanational Agency, Waandaaji wa Vodacom Miss Tanzania 2010, Hashim Lundenga akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya wasicahana Maasai ya Mkoani Arusha jana wakati warembo wa Vodacom Miss Tanzania walipoitembelea shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi.
Balozi wa Kampeni ya Malaria Haikubaliki ambaye pia ni mwanamuziki Mwasiti Almas pamoja na baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimkabidhi chandarua , mmoja wa wagonjwa katika Hospitali ya Mto wa Mbu Mkoani Manyara jana. Warembo wa Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Paulina Lowasa dada wa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowasa, akiwapa mkono wa kuwatakia heri Warembo wa Vodacom Miss Tanzania alipokutana nao Wilayani Monduli mkoni Arusha jana na kuwapa zawadi ya vikoi vya kimaasai warembo wote 30. Warembo hao wanatembelea Kanda ya Kaskazini kuangalia vivutio vya Utalii nchini.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimkabidhi chandarua Sifuni Erasto, mmoja wa wagonjwa katika Hospitali ya Mto wa Mbu Mkoani Manyara jana wakati warembo hao walipombatana na Balozi wa Kampeni ya Malaria Haikubaliki Mwasiti Almas (watatu kulia). Warembo wa Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimkabidhi chandarua Mria Charles, mmoja wa wagonjwa katika Hospitali ya Mto wa Mbu Mkoani Manyara jana wakati warembo hao walipombatana na Balozi wa Kampeni ya Malaria Haikubaliki Mwasiti Almas (watatu kulia). Warembo wa Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Meneja Mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Henry Tzamburakis (kulia) akimkabidhi vyandarua Mganga wa Hospitali ya Mto wa Mbu Mkoani Manyara Frank Sanga jana ambapo Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 waliopo katika ziara ya kutembelea Vivutio vya Utalii Kanda ya Kaskazini. Katikati ni Balozi wa Malaria nchini Mwasiti Almasi.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiwa wameshikilia vyandarua kabla ya kugawa vyandarua kwa baadhi ya wakazi wa mto wa Mbu mkoani Manyara jana. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutuio vya Utalii na kuhamasisha Utalii wa Ndani Nchini.
Mshiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010,Geneviver Emmanuel akigawa chandarua kwa mmoja wa wakazi wa Mto wa Mbu Mkoani Manyara jana katika utekelezaji wa Kapeni ya malaria. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutuio vya Utalii na kuhamasisha Utalii wa NMdani Nchini.

Comments

Post a Comment