VODACOM MISS TANZANIA NDANI YA HIFADHI YA NGORONGORO

Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiangalia Simba anayepita karibu na magari yao jana wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Ngorongoro kujionea wanyama na mambo mbali mbali yalipo katika hifadhi hiyo.

Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakinunua shanga za kimasai kutoka kwa wauzaji waliopo katika Boma lililopo katika Hifadhi ya Ngorongoro wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo wakati wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa nbi sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani jana.

Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakitoka katika nyumba za Tembe za wafugaji wa jamii ya Kimasai waishio katika Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani jana.

Comments