"TUPENI KURA ZENU"




CECY JEREMIAH- UJUMBE


TULLO CHAMBO- UJUMBE

NASONGELI KILYINGA -KATIBU MSAIDIZI

ONESMO KAPINGA

WAGOMBEA wa nafasi mbalimbali za uongozi katika chama cha waandishi wa habari za Michezo Tanzania (TASWA), wameomba wajumbe kuwapigia kura za ndiyo ili kuwawezesha kutwaa nafasi hiyo ambapo wanaamini wataleta mabadiliko makubwa katika uongozi wao.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika keshokutwa katika ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, ambapo nafasi zitakazowaniwa ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mweka Hazina Msaidizi na Wajumbe sita wa kamati ya utendaji.

Wagombea waliojitokeza ni pamoja na Masoud Sanani, Juma Pinto, Mpoki Bukuku (Mwenyekiti), Tom Chilala, Shaffih Dauda, Maulid Kitenge (Makamu Mwenyekiti), Dina Ismail, Sultan Sikilo (Mhazini), Mohamed Mkangara (Mhazini Msaidizi), Cecy Jeremiah, Onesmo Kapinga, Tullo Chambo, Mashaka Mhando, Masau Bwire, Elius Kambili, Salum Jaba, Grace Hoka na Zena Chande wanawania ujumbe.

Comments

  1. mh mi chichemi mamapipiro kumbe nawe umejitosa, kila la heri nakutakia nasubiri matokeo kwa hamu.
    Dafrossa, A- Town

    ReplyDelete
  2. pole na kazi mamaa pipilo, mbona umetubania picha za wagombea wengine?ingekuwa poa kama ungewweka na picha za wengine vili tuwaone jamani tuwape ushauri wa haraka haraka, mdau wa michezo

    ReplyDelete
  3. haya nawatakia uchaguzi mwema na japo si mwanachama hai nakupa kura yangu kivuli ya ndiyo mpe hi cecy mwambie pia tunamtkia ushindi mwema,mdau

    ReplyDelete
  4. Kura au kula, nafikiri hapo ni kura, kwasababu kazi wanayoitaka ina majukumu mazito, na kwahiyo atakayechaguliwa ajue ana kazi nzito!
    Mhh twawatakia kila-laheri nawe mdau mwenzetu naona umo, tunakutakia kila-laheri, ushinde ili utusaidie yale yanayofaa ngazi za juu

    ReplyDelete

Post a Comment