STARS SASA KUKIPIGA NA HARAMBEE


MCHEZO wa Kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Misri uliokuwa uchezwe Agosti 11 nchini Misri umeota mbawa nma badala Stars itamenyana na timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Florian Kaijage sababu za mchezo huo kuota mbawa ni kutokana na TFF kutowasilisha majina ya wachezaji watakaomenyana na Misri kwa Shirikisho la soka la nchi hiyo (EFA) jambo ambalo TFF walilipinga kutokana na sababu kwamba kocha Mkuu wa Stars alikuwa hajawasili.


Kaijage alisema katika mchezo huo Harambee Stars itashirikisha wachezaji wanne wa Kimataifa akiwemo Denis Oliech anayekipiga katika klabu ya Auxerre ya Ufaransa na Mc Donald Malinga anayekipiga katika klabu ya Inter Milan ya Italia.

Aidha Kiajage alisema kambi ya Stars ilianza jana jioni tayari kwa mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo ikiwa ni siku maalum ya Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA).

Comments

  1. ndio teseme, Misri wameiogopa Stars kwa maana imeshawashughulikia wengi na iliitoa jasho Brazil!, waelezeni wasiwaogope Stars

    ReplyDelete
  2. Misri wameiogopa Stars kwa sababu ya rekodi zake za FIFA, waache woga

    ReplyDelete

Post a Comment