SIMBA KUPIMANA UBAVU NA MABINGWA WA KENYA J'MOSI

MWENYEKITI WA SIMBA, ISMAIL ADEN RAGE

RAGE KULIA NA MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA GEOFREY NYANGE 'KABURU' WAKATI WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MAKAO MAKUU YA KLABU HIYO ILIYOPO MTAA WA MSIMBAZI NA TWIGA.

MABINGWA wa soka wa Kenya klabu ya Ulinzi wanatarajiwa kutua nchini kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki na vigogo wa soka nchini Simba na Yanga.

Ulinzi itaanza kucheza na Simba Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa,kabla ya kucheza Yanga Jumapili katika uwanja huo ambapo timu hizo zipo katika maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom.
Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amesema leo  kwamba timu inaendelea vizuri na mazoezi na  kikosi cha timu hiyo kitaondoka kwa ndege septemba 12 kwenda Mwanza kwa ajili ya kuweka kambi yao baada ya kuamua kutumia ueanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Comments

  1. huyo rage mbona anapenda sana kuonekana si wamemwajiri msemaje ebu mwambieni akafanye kampeni huko asijiamini kuna chadema inatisha hivi kwanza huyu si msomali vipi kuhusu uraia wake alijipeleka uhamiaji?

    ReplyDelete

Post a Comment