SIMBA KAMA CHELSEA BWANA!







KOCHA MKUU WA SIMBA PATRICK PHIRI KUSHOTO NA KOCHA WA VIUNGO NA SAIKOLOJIA SYLLERSAID MZIRAY

PHIRI, MZIRAY


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, Simba ya jijini Dar es Salaam, wamesema kufungwa kwao na mahasimu wao Yanga katika Ngao ya Hisani, ni kama vile ilivyokuwa kwa Chelsea ya England, hivyo mashabiki wakae mkao wa kula.


Katika mechi hiyo iliyopigwa jana Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ililala kwa mikwaju ya penalti 3-1.

Msemaji wa Simba, Clifford Ndimbo, alisema wanakichukulia kipigo hicho kama kile walichokipata mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Chelsea, ambao walifungwa 3-1 na Man United, katika Ngao ya Jamii lakini mechi ya kwanza ya Ligi wakapiga mtu 6-0.

Aidha, Ndimbo alisema kukosa penati kwa mastaa wake inatokea hata kwa nyota wengine duniani huivyo haikuwa ni jambo la ajabu.

Ndimbo aliongeza kuwa timu yao ilionyesha kiwango cha hali ya juu katika mechi hiyo lakini bahati haikuwa yao kwa siku ya jana.

Kwa sasa Simbva ianendelea na maandalizi yake ya ligi kuu itakayoanza keshokutwa ambapo Simba itacheza na African Lyon katika uwanja wa Uhuru,jijini Dar es Salaam.

Comments

  1. MAMA PIPIRO WEWE NI SIMBA NINI MAANA UNAVYOIPAMBA, HATA PICHA NYINGI NI ZAO TANGU JUZI, MARA SIMBA KAMA CHELSEA, TUAMBIE JAMANI.
    KWA UPANDE MWINGINE NAWAPONGEZA WACHEZAJI WA SIMBA KWA KUCHEZA VIZUR KATIK MECHI HILE ILA HAIKUWA BAHATI YAO.
    SIMBA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.
    MIMI SIMBA DAMU

    ReplyDelete

Post a Comment