SIMBA BAHATI MBAYA KWA YANGA


WACHEZAJI YANGA WAKIWA NA BAADHI YA VIONGOZI PAMOJA NA NGAO YAO


RAIS WA TFF LEODGER TENGA AKIMPA MKONO WA HONGERA KOCHA WA YANGA KOSTADIN PAPIC

YANGA ya Dar es Salaam mieweza kutwaa ngao ya jamii baada ya kuwafunga kwa penati 3-1 mahasimu wao wa jadi nchini Simba katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Penati hizo zilikuja baada ya dakika tisini kumalizika kwa timu hizo bila ya kufungana.

Hatua ya penati ilianza kwa Ernest Boakye wa Yanga kukosa, kisha akaja Emanuel Okwi wa Simba akakosa, Geofrey Bonny wa Yanga alipata, Uhuru Seleman wa Simb alikosa, Stefen Mwasyika Yanga alipata, Amri Kiemba alikosa kwa Simba, Isac Boakye aliipata ya Yanga na Mohamed Banka alipata ya Simba

Comments