SHIWATA YAWAPOZA WANACHAMA WAKE

MWENYEKITI WA SHIWATA KASSIM TALIB AKIWAONYESHA WANACHAMA MOJA YA VIELELEZO WAKATI WA MKUTANO LEO.



BAADHI YA WANACHAMA WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO ULIOFANYIKA KWENYE UKIMBI WA AFRICENTRE.

MWENYEKITI wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA), amewataka wachamama wa shirikisho hilo kutumia vikao halali badala ya kusikiliza habari za nje za vikao ambazo msingi wake ni kuwavuruga.
Akizungumza na wanachama jijini Der es Salaam jana, Mwenyekiti wa SHIWATA, Kassim Taalib, alisema anaamini kuwa habari zilizotangazwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari, ziliwafanya wanachama wachache waamini kuwa ni kweli, hivyo kuondoa imani kwa viongozi wao.
“Nasisitiza kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, Shiwata ipo na wala hakuna kiongozi yeyote mwenye nia ya kufanya utapeli na wanaofikiria hivyo wamefilisika kimawazo,” alisema Taalib.
Aidha, alisema shirikisho hilo ni la wanachama, lenye lengo la kutetea haki za wasanii na kubuni miradi mbalimbali, ambayo itawaletea mapinduzi ya kweli ya kiuchumi.
Taalib alisema anatambua mtafaruku huo ulisababishwa na baadhi ya wanachama ambao walijiunga na Shirikisho hilo kwa kufuata mkumbo, bila kujua nia halisi.
Aidha aliwahakikishia wanachama kuwa  hawajadhulumiwa, maeneo yao yapo na kwa kudhihirisha hilo, hivi karibuni yataanza kusafishwa na ‘greda’ lililokodishwa kutoka Mkoa wa Pwani.
Taalib alisema, mara baada ya kumalizika kufanyiwa usafi, Shiwata itawaalika viongozi wa kitaifa katika sherehe za uzinduzi.

Comments