SHINDANO LA KUSAKA WABUNIFU LAJA




Kwa mara nyingine tena sekta ya ubunifu Tanzania inatoa fursa kwa wabunifu wote wenye ndoto za kuwa wabunifu bora kushikiri katika shindano la kuibua vipaji vya wabunifu hapa Tanzania . Shindano hili la mwaka limekua likifanyika chini ya mwanvuli wa jukwaa kuu la Africa Mashariki Swahili Fashion Week.

“Tunaangalia wabunifu ambao wana malengo ya kuwa wabunifu bora wa mavazi hapa Tanzania ” Alisema Mustafa Hassanali.

Shindano hili linafanyika kwa mwaka wa tatu sasa, halina kikwazo cha umri, na linatoa fursa kwa watu wote wanaoamini kwamba wana kipaji cha ubunifu, na wanataka kuwa wabunifu. “Swahili Fashion Week ni jukwaa bora kwa wabunifu kuonyesha uwezo wao wa ubunifu na kuibua sindano la wabunifu wapya, ni jukwaa linalowawezesha watu kufikia malengo yao ”, aliongeza Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week.

Shindano hili linatoa fursa kwa wabunifu kutoka pande zote za Tanzania . Mwisho wa kujisajili ni tarehe 30th ya mwezi wa August 2010. “Mwaka 2008 Edwin Musiba alishinda, na mwaka 2009 alishinda 2jenge Afrika Matalay, najiuliza nani atashinda mwaka huu?”, alimalizia Hassanali.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na shindano la ubunifu, tafadhali wasilina na Mratibu wa Swahili Fashion Week bwana Washington Benbella, simu namba 0717 547792 au kupitia barua pepe , designers@swahilifashionweek.com

Comments