ROCK CITY MARATHON KUFANYIKA MWANZA SEPTEMBA 26

KATIBU WA CHAMA CHA RIADHA TANZANIA (RT) SULEIMAN NYAMBUI (KUSHOTO) AKIFAFANUA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI WAKATI WA UZINDUZI WA MBIO ZA ROCK CITY MARATHON KATIKATI NI MRATIBU WA MBIO HIZO RAYMOND KANYAMBO NA KULIA NI MKURUGENZI WA MASOKO WA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB) AMANTI MACHA.



WANAHABARI
KAMPUNI ya Capital-Plus International (CPI) imeandaa mashindano ya riadha ya
kilomita 21 yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2010’ yatakayofanyika
Septemba 26 mwaka huu Jijini Mwanza.
Tunafanya mashindano haya kwa mara ya pili ambapo ya kwanza yalifanyika mwaka
jana na kwamba tunatarajia mbio hizo zitaanzia uwanja wa CCM Kirumba kuelekea
njia tofauti za Jiji la Mwanza na kumalizia katika uwanja huo.
Kama ilivyokuwa katika mashindano yaliyopita tunatarajia wanariadha kutoka
sehemu mbalimbali mchini pamoja na nchi jirani watashiriki katika mashindano
hayo ya aina yake katika ukanda huo wa Ziwa.
Mialiko kwa ajili ya ushiriki wa nchi jirani tayari imetumwa kupitia vyama vya michezo husika ambavyo ni Jamhuri ya watu wa Congo (DRC), Rwanda, Burundi,
Kenya,Uganda na Zambia.
Mashindano haya pamoja na mbio hizo ndefu pia yatahusisha matukio mengine kadhaa
ambayo ni mbio za kilomita 5 kwa wote , mbio za kilomita 3 kwa wazee wa kati
ya umri wa miaka 55 na zaidi, mbio za kilomita 3 kwa watu wenye ulemavu na mbio
za kilomita 2 kwa watoto wa kati ya umri wa miaka 7 -10.
Ada za ushiriki kwa mashindano haya ni sh. 500/= kwa mbio ndefu za kilomita 21,
sh.300/= mbio za kilomita 5 na 3 wakati mbio zitakazohusisha watoto ni bure.
Tumeamua kupanua wigo wa ushiriki mwaka huu kutokana na kutambua umuhimu wa
michezo kwa rika mbalimnbali lakini muhimu zaidi ni mapendekezo tofauti
tuliyopokea kupitia wadau mbalimbali baada ya kumalizika kwa mashindano ya mwaka
jana.
Mashindano haya yamedhaminiwa na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL),Mfuko wa
Pensheni wa Taifa (PPF), Hoteli ya New Africa, NSSF Clouds FM na Isamilo Lodge
ya Mwanza.
Fomu kwa ajili ya kujisajili zinapatikana Isamilo Lodge Mwanza, Ofisi za uwanja
wa CCM Kirumba, Ofisi za Capital- Plus International Limited- DSM, Makao Makuu
ya Chama cha Riadha Tanzania (RT) Dar es Salaama, Ofisi za RT Mwanza.
Pia washiriki wanaweza kupata fomu hiyo katika www.capitalplus.co.tz /
rockcitymarathon.com

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi kuhusiana na mashindano haya unaweza kutuandikia

kupitia info@capitalplus.co.tz.

Comments